Mtaalam

Mbosso

Compositor: Não Disponível

Na Mbosso Khan tena
(Sounds by Abbah)

Una kila sababu
Ya kusimama kimaso maso
Mungu kweli wa ajabu
Kanionyesha kwa yangu macho
Chukua zangu swahabu
Mi nibaki na dhambi zako
Unishikishe adabu
Mida ya kulala nitokwe jasho
Mi sijui kupigna mwili wangu wa mapensi dear
Tusipende kugombana mi mwepesi kulialia
Si kujibanabana, raha ya penzi kujiachia
Wako mahututi mama, nimekufa nimejifia
Eeeh! Nalambishwa asali
Kwenye mzinga wa nyuki, tamu ni hatari
Nalambishwa asali
Nachezeshwa buzuki, dudu chalichali

Nimempata!
Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata mtaalamu nimempata
Nimempata mtaalamu nimempata

Mi mTanzania wa halali, ila chembechembe za India
Mungu kaninyima ufahari, ila kwa huba najisifia
Sitakuhonga magari, ila mahaba utasanzia
Penzi kachumbari kwa ugali na pilipili ya kushagia
Aah eeh! Nikuite nani?
Majina yote nishamaliza

Aah eeh! Wangu wa ubani
Umeweza kunituliza
Aah eeh! Mambo ya chumbani
Yaani nalala huku napulizwa
Aah eeh! Penzi zito tani
Napewa raha kupitiliza

Eeeh! Nalambishwa asali
Kwenye mzinga wa nyuki, tamu ni hatari
Nalambishwa asali
Nachezeshwa buzuki, dudu chalichali
Nimempata! Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata! Nimempata mtaalam nimempata

Mtaalamu wa mapenzi
Nimempata mtaalamu nimempata
Fundi wa mafundi kungwi
Nimempata mtaalamu nimempata
Wasafi

©2003- 2025 lyrics.com.br · Aviso Legal · Política de Privacidade · Fale Conosco desenvolvido por Studio Sol Comunicação Digital